Jumanne, Januari 28, 2014

Barkhad Abdi ambaye ameigiza kama Abduwali Muse Kiongozi wa Kundi la Maharamia katika Filamu ya Captain Philips.

Hii ni moja ya Kipande alichoigiza  Barkhad Abdi mara baada ya kufanikiwa kuingia kwenye Meli ya MV Maersk Alabama.



Filamu ijulikanayo kama Captain Philips ni Moja ya Filamu iliyotoka mnamo tarehe 11 Ocktoba 2013, Filamu hii imeongozwa na muongozaji mahiri kabisa kutoka Hollywood aitwaye Paul Greengrass. Pamoja na Kuiongoza Vyema Filamu hiyo lakini filamu hiyo ni moja ya filamu iliyotumia Kiasi cha Dola Za Kimarekani Milioni 55.

Filamu hii ya Captain Philips Imeandikwa kutoka kwenye kitabu Kijulikanacho kama "A Captain's Duty: Somali Pirates, Navy SEALs, and Dangerous Days at Sea" ambacho kimeandikwa na Richard Phillips pamoja na Stephan Talty. Filamu hii imetengenezwa kutokana na Tukio halisi la kutekwa kwa Meli ya MV Maersk Alabama Mnamo mwaka 2009 na kupelekea Nahodha wa Meli hiyo  iliyotekwa mnamo 2009 Captain Richard Philips kushikiliwa na maharamia kwa kile kinachodaiwa Kuwa Wabadilishane ili kuweza kulipwa Pesa za Kimarekani.

Ni Filamu iliyochezwa na Tom Hanks kama ndie captain Philips huku akikinzana na Muigizaji mahiri mwenye Asili ya Somalia Barkhad Abdi ambaye alitumia jina la  Abduwali Muse kama kiongozi wa Maharamia ambaye Mwishoni aliweza kushikiliwa na Jeshi la Maji la Marekani baada ya kudanganywa kupanda kwenye meli ya Kijeshi ya Marekani ijulikanayo kama USS Bainbridge kwaajili ya kukubalia juu ya Kiasi cha Pesa walichokuwa wakikitaka kwaajili ya kumuachilia Captain Philips ambaye walimshika Mateka. USS Bainbridge ni meli ya kijeshi ambayo ilikuja kutoa msaada mara baada ya Captain Philips Kuomba Msaada katika Kituo Cha Kijeshi cha Majini Kinachopamba na Maharamia kilichopo Dubai.

Ni moja ya Filamu ambayo kikukweli ukiitazama kwanza huwezi kuboreka, Pili rangi iliyotumika katika Filamu hiyo Ni Nzuri sana , Huku sauti zikiwa zinasikika vizuri kabisa.

Lugha zilitumiwa katika filamu hii ni Kiingereza na Kisomali.

Ufuatao ni Wasifu wa Muigiza Barkhad Abdi ambaye aliigiza kama Abduwali Muse kiongozi wa Maharamia walioteka Meli ya MV Maersk Alabama

Jina kamili: Barkhad Abdi
Amezaliwa: April 10, 1985
Makazi yake: Minneapolis, Minnesota
Uraia: Mmarekani Mwenye Asili ya Kisomali
Kazi yake: Muigizaji, Mtayarishaji na Muogozaji wa Filamu na Muziki

Tuzo alizowahi kuchukua ni Kama Capri Breakout Actor Award, Indiana Film Critics Association Award for Best Supporting Actor, Boston Society of Film Critics Award for Best Supporting Actor (2nd place), Dallas-Fort Worth Film Critics Association Award for Best Supporting Actor (3rd place), National Society of Film Critics Award for Best Supporting Actor (3rd place) na nyingine Nyingi tu.

Kabla ya Kuingia kwenye Tasnia ya Filamu Barkhad Abdi alikuwa ni Dereva na Mtunza store ambaye alijiajili mwenyewe katika Biashara ya Mawasiliano ambapo ofisi zake zilikuwa katika Jengo la Marekani (Mall of America) akiwa pamoja na kaka yake Guled Abdi.

0 comments:

Chapisha Maoni