Jumamosi, Februari 01, 2014

Kelvin akiwa hospitalini baada ya kuokolewa na wenzake alipopambana na chatu aliyetaka kummeza.

Raia mmoja mkazi wa Mwinilunga nchini Zambia ameponea chupu chupu kufa baada ya kuvamiwa na chatu.

Kelvin Katoka ambaye ni dereva wa malori yanayochimba mchanga katika machimbo ya Copa alirukiwa na chatu huyo mkubwa na kuanza kumzungurusha kwa nia ya kuanza kummeza mzima mzima.

Hata hivyo, Kelvin alipambana na chatu yule kwa kumng'ata sehemu mbali mbali za mwili wake bila mafanikio.Kelvin mwenye umri wa miaka 25 tu alijitahidi kuchomoa kisu mfukoni na kulichoma joka hilo mara kadhaa kabla hajaishiwa nguvu na kupoteza fahamu wakati ambapo bado chatu huyo akiwa ameshaanza kumminya na kuanza kummeza.

Wakati ambao Kelvin yupo hoi bin taaban kutokana na sumu ya nyoka huyo ndipo wafanyakazi wenzake wawili walipopita katika eneo hilo na kumuua nyoka huyo na kumkimbiza Kelvin Hospitalini.Hata hivyo bado Kelvin yu mzima na anaendelea vizuri na matibabu.

0 comments:

Chapisha Maoni