Jumapili, Januari 26, 2014



Abiria 17 akiwemo waziri wa katiba na sheria Zanzibar Mhe. Abubakari khamis bakar, na marubani wawili, wamesalimika kifo baada ya ndege ya shirika la ndege la ‘Zanz air’ kufeli breki, muda mfupi wakati ndege hio ilipo kuwa ikitua  kwenye uwanja wa ndege wa Abeid amani karume, uliopo nje kidogo ya mji wa chakechake mkoa wa kusini Pemba


Kwamujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa polisi mkoa kusini Pemba  kamishina msaidizi  swalehe mohamed swalehe na kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo wakati wa kutua ilipata ikhitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje ya uwanja  umbali wa mita miambili kwenye vichaka

 Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie juruhiwa    licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa nakisha kusimama baada ya ringi kujizonga namizizi ya pori hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni