Kipaji: Rogerio Holanda akipozi kwenye picha na vinyago vya nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo.
MTAALAM wa uchongaji nchini Brazil, Rogerio Holanda ameonekana kufarahia fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini mwake baada ya kutumia matunda aina ya matiki maji kuchonga vinyago viwili vyenye picha ya wachezaji wake kipenzi, Cristiano Ronaldo na Neymar .
Holanda ameonekana akifanya jitihada kubwa kuchonga picha za Ronaldo kwa kutumia matikiti maji aliyoweka katika mabakuli makubwa mawili, huku akitumia nembo ya kibiashara ya nyota huyo wa Real Madrid, `CR7`.
Mchongaji huyo mwenye kipaji kikubwa, pia amechonga vinyago nyota wa Brazil, Neymar kwenye matiki maji ndani ya hoteli ya San Raphael hotel mjini Sao Paulo.
Jamaa akifanya kazi yake ndani ya hoteli ya San Raphael, mjini Sao Paulo .
Holanda anaamini Ronaldo atakuwa fiti kusafiri kwenda Brazil, baaada ya nyota huyo kutolewa nje katika mchezo wa La Liga wa sare ya 1-1 dhidi ya Valladolid kutokana na kupata majeruhi ya nyama za paja.
Bosi wa Madrid, Carlo Ancelotti amempumzisha Ronaldo mpaka kwenye mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya watani zao wa mji, Atletico Madrid, mei 24 mwaka huu, lakini sare waliyopata ilipunguza matumaini yao ya kuwaa ubingwa wa La Liga.
Sergio Ramos alivaa viatu vya Ronaldo baada ya kufunga bao dakika ya 25 kwa mpira wa adhabu ndogo, lakini bao la beki huyo lilisawazishwa dakika ya 85

Holanda akifanya kazi ya kuchonga vinyago vya Neymar na Ronaldo
0 comments:
Chapisha Maoni