Umati wa wakazi wa kijiji cha uchunga wakitazama ajali ya fuso.
Watu 3 wamekufa na wengine zaidi ya 47 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda mnadani kupinduka wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea asubuhi katika eneo la uchunga wilayani humo baada ya gari hilo haina ya fuso namba T680 ARL kuacha njia na kupinduka.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na derava wa gari hilo aliyetambulika kwa jina la Shija Ngassa amekimbia baada ya ajali hiyo.
Ajali hiyo ya fuso imesababisha vifo vya watu watatu ambapo moja ametambulika kwa jina la Difa Shimo mili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Jastus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Kamugisha amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na kumsaka dereva wa gari hilo sanjari na kutoa onyo kwa wafanya biashara wa minadani kuacha kupanda magari ya mizigo.
0 comments:
Chapisha Maoni