Jumamosi, Juni 07, 2014

Kyle Jones, mwenye umri wa miaka 31 ameamua kumchumbia bibi mwenye umri wa miaka 91 huku akidai kuenjoy zaidi mapenzi ya bibi huyo.

Kijana huyo wa Pittsburgh, Pennsylvania ameeleza kuwa tayari ameshamtambulisha bibi huyo kwa mama yake mzazi ambaye yeye ana miaka 50, na mama ameridhia.

mzee na kijanaKwa mujibu wa Metro wa Uingereza, kijana huyo ameeleza kuwa amekuwa katika uhusiano na bibi huyo kwa muda wa miaka mitano hadi sasa.

Wawili hao wameonekana katika mitaa mbalimbali wakizunguka huku bibi huyo akiwa amevaa nguo za kisasa.

Kyle ameeleza kuwa anashangaa kusikia watu wanasema wazee wenye umri sawa na wa bibi huyo huwa hawaenjoy kufanya mapenzi, lakini kwake ni tofauti.

Kyle ambaye anahistoria ya kuwa na wapenzi wazee, ameeleza kuwa kama wanaume wengine wanavyochagua wanawake, yeye anapenda zaidi wanawake wazee.

Bibi huyo ameeleza jinsi ambavyo kijana huyo alimpata. Anadai aliipata namba yake ya simu na akaanza kuwa anampigia mara kwa mara na mwisho wakaanza uhusiano.

tazama video kwa kubofya play hapa chini... 

0 comments:

Chapisha Maoni