Nyota wa mchezo: Sir Alex Ferguson akimpatia zawadi Angel Di Maria kama mchezaji bora wa mechi.
Sir Alex Ferguson alishindwa kuvumulia katika mchezo wa jana baada ya winga wa Real Madrid, Angel di Maria kuonesha kiwango cha juu na kuamua kumpa zawadi ya mchezaji bora wa mechi ya fainali ya UEFA mwaka huu.
Gwiji huyo wa Manchester United alivutiwa sana na kiwango cha Di Maria katika mchezo wa jana na kuisaidia Real Madrid kushinda mabao 4-1 dhidi ya majirani zao, Atletico Madrid, mjini Lisbon.
Akikimbiza: Di Maria alikuwa nguzo ya Real Madrid usiku wa jana mjini Lisbon
Muda wa sherehe: Muargentina huyo alifanya kazi kubwa kuwasaidia Real Madrid kutwaa ndoo yao ya 10 ya Ulaya.
0 comments:
Chapisha Maoni