Jumamosi, Mei 31, 2014

 Marehem George Tyson enzi za uhai wake.
Kwenye watu ambao wana mkono mkubwa kwenye filamu Tanzania basi na huyu ni miongoni mwao, amehusika kwenye movie nyingi sana zikiwemo za mke wake ambae ni mwigizaji Monalisa kama ile ya ‘Girlfriend’ aliyocheza na kina GK, T.I.D Ay na wengine miaka hiyo.
 
Kuanzia saa tatu usiku wa May 30 2014 zilianza kusambaa taarifa kwamba Director George Tyson amefariki dunia ila sasa ndio zimethibitika kuwa ni rasmi ambapo Mwigizaji Wema Sepetu na mtangazaji Zamaradi Mketema ni miongoni mwa waliopata uthibitisho.

Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha  The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu.


 George Tyson akiwa na Mboni waliyepata nae ajali.

Wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu walipata nafasi ya kuonyesha majonzi yao kwa kuposti katika kurasa zao za Instagram na Twitter.

Chukua time yako kuangalia baadhi ya post za wasanii hao hapa chini...





Kwa taarifa zaidi ingia HAPA

Tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi....RIP brother 












0 comments:

Chapisha Maoni