MAUMIVU! Mfugaji wa jamii ya Kimasai, Sita Lumembe (36), mkazi wa Kijiji cha Ludewa wilayani Kilosa mkoani hapa, amefikishwa hospitalini akiwa hoi baada ya kupigwa pembe la tumbo na mmoja wa ng’ombe wake aliokuwa akiwachunga.
Mfugaji wa jamii ya Kimasai, Sita Lumembe (36), mkazi wa Kijiji cha Ludewa wilayani Kilosa mkoani Morogoro aliyepigwa pembe la tumbo na mmoja wa ng’ombe wake aliokuwa akiwachunga.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri hivi karibuni katika kijiji hicho ambapo jamaa huyo alikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kilosa anakoendelea na matibabu hadi sasa.
Akilisimulia Ijumaa Wikienda mkasa mzima, kaka wa Sita aliyejitambilisha kwa jina la Ole Lumembe alisema mdogo wake alikumbwa na tatizo hilo kwenye kijiji hicho alipowapeleka ng’ombe wake malishoni.
“Ng’ombe wake mmoja aliyekuwa na ndama alimpiga na pembe tumboni, akaanguka na kupoteza fahamu.

Baadhi ya jamaa zake wakimchukua kwa ajili ya kumpatia huduma.
“Wasamaria wema walinipigia simu, nikafika eneo la tukio na kukodi bodaboda iliyomkimbiza hospitalini.
“Baada ya daktari kumcheki, alikimbizwa wodini kwani damu ilikuwa ikimwagika kwa wingi kutoka tumboni,” alisema Lumembe akiwa na huzuni. Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kilosa, Christopher Chiweka alithibitisha kumpokea mgonjwa huyo.
“Alifikishwa akiwa na hali mbaya mno hivyo tukamkimbiza wodini kwa uchunguzi zaidi, sambamba na matibabu anayoendelea nayo,” alisema daktari huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni