Jumapili, Mei 25, 2014

Anaweza kurudi? Mario Balotelli anaweza kurudi ligi kuu soka nchini England akiwa na  Liverpool au Arsenal.

MSHAMBULIAJI mtukutu wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli anaweza kurudi tena ligi kuu soka nchini England, huku Asernal na Liverpool zikionesha nia ya kutaka kumsajili.

Nyota huyo ambaye haishiwi vituko amechoka na ubaguzi wa rangi unaokumbana nao Italia na inafahamika kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City ametambua kuwa maisha ya England hayakuwa mabaya sana.

Arsenal wapo katika mazungumzo na Real Madrid ili wamsajili Karim Benzema, pia wanatarajia kuzungumza na watu wa  Balotelli.

Liverpool wataenda kwa Balotelli endapo  Luis Suarez ataondoka kujiunga na Real Madrid au Barcelona baada ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

0 comments:

Chapisha Maoni