Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitoa muhadhara katika Chuo Kikuu cha Taaluma ya Sera 'GRIPS'
wakati alipoalikwa kwenye muhadhara huo uliofanyika chuoni hapo Jijini
Tokyo Japan, jana Mei 23, 2014.
Baadhi ya wanachuo kutoka mataifa mbalimbali wa Chuo hicho waliohudhuria
Muhadhara huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati
alipokuwa akitoa muhadhara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini
Japan, waliohudhuria Muhadhara huo baada ya kumalizika kwa muhadhara huo
katika Chuo Kikuu cha Taaluma ya Sera 'GRIPS' Jijini Tokyo Japan, jana
Mei 23, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na baadhi ya wanachuo Watanzania, wanaosoma katika Chuo
hicho baada ya kumalizika kwa Muahadhara huo jana Mei 23, 2014, jijini
Tokyo Japan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachuo Watanzania
wanaosoma katika Chuo hicho cha Taaluma ya Sera 'GRIPS' Jijini Tokyo
Japan, jana Mei 23, 2014, baada ya kumalizika kwa muhadhara huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amesema nchi zinazoendelea hususan za Kiafrika bado zinahitaji uwekezaji zaidi vitega uchumi kutoka nje (FDIs) ili kupata maendeleo ya haraka na kuondokana na umaskini.
Dkt. Bilal ameyasema hayo leo (Mei 23, 2014) wakati akitoa muhadhara kuhusu Mtazamo wa Nchi Zinazoendelea na Changamoto za Uwekezaji Vitega Uchumi vya Nje na Hatma yake katika Kuondoa Umasikini kwa kutumia mfano wa Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Uchanganuzi wa Sera (GRIPS) mjini Tokyo.
Alisema Afrika inahitaji misaada zaidi itakayosadia kukuza teknolojia itakayowawezesha Waafrika kuvuna maliasili ambazo hazijavunwa. Aliongeza kuwa hii ndiyo njia pekee itakayoliwezesha Bara la Afrika kuongeza mapato na kuchangia maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.
Alisisitiza kuwa uwekezaji unaohitajika zaidi ni katika sekta za za madini, mafuta na gesi, kilimo na vyanzo vingine vya nishati kama vile nishati ya jua na upepo. Alisema sekta hizo ndizo zinazohitaji teknolojia ya kisasa kutoka mataifa yaliyoendelea ili kurahisisha uvunaji wake.
Wakichangia hoja hiyo, wanafunzi wa chuo hicho walihoji namna Tanzania inavyojiandaa kuhakikisha upatikanaji wa mafuta na gesi hauwezi kuathiri amani na utulivu wa nchi yetu. Makamu wa Rais aliwaeleza kwamba utafutaji, uchimbaji na usambaji unafanyika katika misingi ya uwazi ili Serikali na kila mwananchi aelewe ni kwa namna gani atakavyonufaika na rasimiali hiyo.





0 comments:
Chapisha Maoni