Tairi ya bajaji hiyo likiwa limekatika.
Askari wa usalama barabara wakikagua ajali hiyo iliyosababisha hadi ukuta wa uzio wa bustani ya Manispaa ya Iringa kubomoka.
Bajaji ikiwa imepata ajali mchana huu eneo la posta mjini Iringa.
Bajaji ya Mng'aro wa sembe akiwa emepata ajali wakati ikisambaza unga huo.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo mbaya.
Maneno ya maudhi yaliyoa ndikwa nyuma ya Bajaji 'FUATA YAKO" nusuru yamtokee puani dereva
BINTI mmoja ambae ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari mjini Iringa amejeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na Bajaji ya kampuni ya unga ya Mng'aro wa Sembe ya mjini hapa.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 8.35 mchana wa leo katika eneo la Posta barabara ya Iringa- Dodoma wakati Bajaji hiyo ikitokea eneo la Kihesa kuja mjini Iringa.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao dereva wa bajaji .
Kwani alisema iwapo dereva huyo angekuwa katika mwendo wa kawaida ajali hiyo isingetokea.
Hata hivyo mashuhuda hao akiwemo Bw Mashaka Kayoka ambae ni mmoja kati ya wauza magazeti maaarufu eneo hilo la posta alisema kuwa binti huyo ni mtu pekee aliyejeruhiwa japo eneo hilo huwa wanashinda watu wenye ulemavu wa viongo wakijishughulisha kwa biashara ila wamenusurika .
Mbali ya mwanafunzi huyo kujeruhiwa hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa na dereva wa bajaji hiyo amekamatwa .
0 comments:
Chapisha Maoni