Leo February 17 kutoka Mhakama kuu kanda ya Dar es salaam,msanii wa
maigizo nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu Lulu alikuwa akisomewa
shitaka lake la kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Steven
Kanumba April 07 2012 eneo la Vatican.
Akisoma maelezo ya awali wakili wa serikali Monica Mbogo mbele ya Jaji
anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba amesema mshtakiwa siku ya tukio
kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mshtakiwa na baadaye mshtakiwa
aliondoka usiku wa saa sita baada ya marehemu kuanguka chumbani ambapo
alfajiri ya february 07 majira ya saa 11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo
la Bamaga.
Kwa upande wake wakili Peter Kibatala ambaye anamtetea Lulu amesema
wameridhishwa na sehemu kubwa ya maelezo ya awali ya mteja wao, ambapo
kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa tena huku kila upande
ukitarajia kuleta mashahidi watatu.
0 comments:
Chapisha Maoni